SHULENI – Opiq
1 / 18
×
Chapter 1.1 (Kiswahili 2)
Kiswahili Mufti Gredi ya 2 (Longhorn Publishers)
Chapter 1.1

SHULENI

Mkiwa wawili, tazameni mchoro huu.

Maswali

  1. Unaona nini katika mchoro huo.
  2. Watu hufanya nini shuleni?
  3. Ukienda shuleni utawaona nani?
  4. Utapata vitu gani shuleni?
  5. Wewe unasoma katika shule gani?
  6. Shule yenu ina vifaa gani?

Sauti na majina ya herufi za Kiswahili.

Sauti /g/

Mkiwa wawili, tazameni michoro hii.

a

Maswali

  1. Taja majina ya michoro hiyo.
  2. Tamka herufi ya kwanza ya majina hayo.
  3. Tamka sauti /g/ baada ya mwalimu.
  4. Tamkeni sauti /g/ mkiwa wawili.
  5. Tamka sauti /g/ peke yako.

Zoezi

Mkiwa wawili, jibuni maswali haya.

  1. Andika herufi g katika daftari lako.
  2. Andika herufi G katika daftari lako.
  3. Tamka sauti /g/ kwa usahihi.

Silabi za herufi g

Mkiwa wawili, tamkeni irabu hizi.

Mkiwa wawili, tamkeni silabi hizi zenye sauti /g/.

Tamka silabi hizi na maneno yenye sauti /g/.

gazeti

Zoezi

Tambua maneno yenye sauti /g/ katika kila sentensi.

Mfano: Gunia limejaa matunda.
Jibu: Gunia
  1. Rula
    yangu
    ni
    ndogo
    .
  2. Baba
    amenunua
    godoro
    .
  3. Nani
    atacheza
    gitaa
    ?
  4. Babu
    anasoma
    gazeti
    .
  5. Hili
    ni
    gereza
    .

Mkiwa watatu, tamkeni maneno haya.

Please wait