Chapter 1.1 (Kiswahili 6)

Kusikiliza na Kuzungumza. Matamshi bora (sauti d,nd,ch na sh)

Silabi na vitanzandimi vya sauti d na nd

  1. Je, unayajua maneno gani yenye silabi za sauti d na nd? Mtajie mwenzako.
  2. Mkiwa katika vikundi kama mtakavyoelekezwa na mwalimu wenu, undeni na mzitamke silabi za sauti d na nd. Fuateni mfano ufuatao:

sauti ya konsonanti

d

d

d

d

d

sauti za vokali

a

e

i

o

u

silabi za sauti d

da

de

di

do

du

  1. Sikilizeni silabi za sauti d na nd zikitamkwa na mwalimu wenu.
  2. Sikilizeni maneno yafuatayo yaliyo na silabi za sauti d na nd yakitamkwa na mwalimu wenu:
    1. dada, ndani
    2. debe, ndevu
    3. dirisha, ndimu
    4. dobi, ndoto
    5. dunia, nduru
    6. duka, ndugu.
  3. Tamkeni majina ya picha zifuatazo:
dawa
ndama
debe
ndege
diski
ndizi
donati
ndoo
dubu
ndusi
  1. Tambueni na mzitamke silabi za sauti d na nd katika majina mliyoyatamka katika Shughuli ya 5.
  2. Mkiwa wawiliwawili, tamkianeni maneno mengine yenye silabi za sauti d na nd mnayoyajua.
  3. Je, unavijua vitanzandimi vyovyote vyenye silabi za sauti d na nd? Wakaririe wenzako vitanzandimi hivyo.
  4. Sikilizeni vitanzandimi hivi vikikaririwa na mwalimu wenu.
    1. Fundi stadi ameliunda dawati maridadi na kuliingiza ndani ya darasa.
    2. Dada Rukia amenunua: dafu, andazi, degi, tende, dishi, ndizi, dodoki, ndoo, dugu na ndusi.
    3. Dobi aliibeba ndoo na dodoki kisha akaondoka na kwenda madobini.
    4. Dada Farida hakulidandia daladala kwa kuwa daima kulidandia daladala ni hatari.
    5. Aliokota maembedodo yaliyodondoka na kuyaweka katika ndoo ndogo iliyokuwamo ndani ya gari dogo.
  5. Tambueni na mzitamke silabi za sauti d na nd katika vitanzandimi mlivyovisikiliza katika Shughuli ya 9.
  6. Karirianeni vitanzandimi vya Shughuli ya 9.
  7. Undeni vitanzandimi vyenye silabi za sauti d na nd.
  8. Karirini vitanzandimi mlivyoviunda katika Shughuli ya 12 mbele ya wenzenu ili wavitolee maoni na waviboreshe.
  9. Katika wakati wako wa ziada, unda vitanzandimi vyenye silabi za sauti d na nd. Viandike vitanzandimi hivyo kwenye tarakilishi au daftarini.
  10. Watumie wenzako kwa baruapepe au uwape daftari lenye vitanzandimi ulivyoviunda katika Shughuli ya 14 ili waviboreshe na kuvikariri.

Silabi na vitanzandimi vya sauti ch na sh

  1. Je, unayajua maneno gani yenye silabi za sauti ch na sh? Mtajie mwenzako maneno hayo.
  2. Mkiwa katika vikundi kama mtakavyoelekezwa na mwalimu wenu, undeni na mzitamke silabi za sauti ch na sh. Fuateni mfano ufuatao:

sauti ya konsonanti

ch

ch

ch

ch

ch

sauti za vokali

a

e

i

o

u

silabi za sauti ch

cha

che

chi

cho

chu

  1. Sikilizeni silabi za sauti ch na sh zikitamkwa na mwalimu wenu.
  2. Sikilizeni maneno haya yaliyo na silabi za sauti ch na sh yakitamkwa na mwalimu wenu:
    1. chaki, shaki
    2. cheka, sherehe
    3. chimba, shiba
    4. chora, shona
    5. chuo, shupavu
    6. chuma, shume.
  3. Tambueni na mzitamke silabi za sauti ch na sh katika maneno mliyoyasikiliza katika Shughuli ya 4.
  4. Tamkeni majina ya picha zifuatazo:
chapati
shati
cherehani
shepe
chipsi
shilingi
chokoleti
shoka
chupa
shuka
  1. Tambueni na mzitamke silabi za sauti ch na sh katika majina mliyoyatamka katika Shughuli ya 6.
  2. Mkiwa wawiliwawili, tamkianeni maneno mengine yenye sauti ch na sh mnayoyajua.
  3. Je, unavijua vitanzandimi vyovyote vyenye silabi za sauti ch na sh? Wakaririe wenzako vitanzandimi hivyo.
  4. Sikilizeni vitanzandimi hivi vikikaririwa na mwalimu wenu.
    1. Alishuka akalichukua shuka lenye picha ya shoka kabla ya sherehe ili lisichezewe na kuwa chafu.
    2. Wanachama wa chama cha shirika la mashamba wameyachimba mashimo katika sehemu chache za mashamba yao.
    3. Wapishi wachache wacheshi shereheni wamekamilisha kukitayarisha chakula chema na cha kutosha.
    4. Usimwache mtoto mchanga awashe cheche za moto zinazoweza kuchacha na kusababisha maafa.
    5. Mshonaviatu hakuchoka kushiriki kuyachimba mashimo ya kutupia taka ili zisichomwe na kusababisha moshi unaoyachafua mazingira.
  5. Tambueni na mzitamke silabi za sauti ch na sh katika vitanzandimi mlivyovisikiliza katika Shughuli ya 10.
  6. Karirianeni vitanzandimi katika Shughuli ya 10.
  7. Undeni vitanzandimi vyenye silabi za sauti ch na sh.
  8. Karirini vitanzandimi mlivyoviunda katika Shughuli ya 13 mbele ya wenzenu ili wavitolee maoni na kuviboresha.
  9. Katika wakati wako wa ziada, unda vitanzandimi vyenye silabi za sauti ch na sh. Viandike vitanzandimi hivyo kwenye tarakilishi au daftarini.
  10. Watumie wenzako kwa baruapepe au uwape daftari lenye vitanzandimi ulivyoviunda katika Shughuli ya 15 ili waviboreshe na kuvikariri.
Please wait