sauti f na v, s na z, l na r, na th na dh
Shughuli 1: Kutambua silabi
1. Tazameni picha hizi mkiwa wawiliwawili. Mweleze mwenzako umeona nini.
fu
vi
sa
zi
li
ro
dha
the
2.
(a) Tamka maneno yafuatayo ukiwa na mwenzako:
figa vuna ugali sahani thelathini | kiazi samaki tangawizi karoti | jokofu maharagwe pilipili dhuru |
(b) Mwonyeshe mwenzako silabi za sauti f na v, s na z, l na r, th na dh katika maneno uliyotamka.
Shughuli 2: Kutamka silabi
1. Ukiwa na mwenzako, tamkeni silabi zifuatazo kwa zamu:
(a) Silabi za sauti f na v fa, fe, fi, fo, fu va, ve, vi, vo, vu | (c) Silabi za sauti l na r la, le, li, lo, lu ra, re, ri, ro, ru |
(b) Silabi za sauti s na z sa, se, si, so, su za, ze, zi, zo, zu | (d) Silabi za sauti th na dh tha, the, thi, tho, thu dha, dhe, dhi, dho, dhu |
2. Elekezwa na mwalimu au mwenzako kutamka silabi zile zinazokutatiza.
Shughuli 3: Kutamka vitanzandimi
Ukiwa na mwenzako, tamkeni vitanzandimi vifuatavyo kwa zamu:
- Fatiha alivua na kufua vazi alilovaa.
- Mvuvi mvivu alishindwa kufunga nyavu za kuvua.
- Kasa wa ziwani amejikaza kisabuni.
- Mzee wa sita alisita kusoma saa zote.
- Shirika la reli larejelea shughuli zake rasmi.
- Hili ni trela na lori la Lolwe.
- Dhamira thabiti ni dira dhahiri maishani.
- Kidhibitimwendo madhubuti ni cha thamani.
Shughuli 4: Kuunda vitanzandimi
Shirikiana na mwenzako kuunda vitanzandimi ukitumia maneno haya:
(a) vua/fua | (c) kura/kula |
(b) sisi/zizi | (d) thamani/dhamani |
Changamka
Tumia kifaa cha kidijitali kama vile simu kujirekodi ukitamka vitanzandimi kisha usikilize utamkaji wako. Mpe mlezi wako pia asikilize matamshi yako.
Chora mchoro huu daftarini kisha ujitathmini.
ndiyo | Ninaweza kwa kiasi kidogo. | Ninahitaji kufanya mazoezi zaidi. | |
Ninaweza kutamka vitanzandimi. |