Maamkuzi
Mwalimu na mwanafunzi wanaamkuana.
Mwanafunzi anasema: “Waambaje mwalimu?”
Mwalimu anajibu: “Sina la kuamba.”
Mwalimu anaendelea kusema: “U hali gani?”
Mwanafunzi anajibu: “Sijambo mwalimu.”
Kisha mwalimu anauliza: “Habari ya nyumbani?”
Naye mwanafunzi anajibu: “Nyumbani tu salama.”
Baadaye mwalimu atakapowaaga wanafunzi jioni atasema: “Alamsiki.”
Wanafunzi nao watamjibu: “Binuru.”
Kisha, mwalimu atawaambia: “Tutaonana kesho.”
Nao wanafunzi watajibu: “Inshallah”.
Zoezi
1. Jibu maamkizi yafuatayo:
- Je, salama?
- Mwambaje?
- Habari za utokako?
- Kwaheri.
- Umeamkaje?
- Umeshindaje?
- Hujambo?
- Hamjambo?
- Habari za jioni?
- Sabalkheri!
- Lala salama/unono!
- Nyumbani hakujambo?
- Kaka ameshindaje?
- M hali gani?
- Masalkheri!
2. Igizeni maamkuzi ya mwalimu na mwanafunzi.
Maelezo zaidi
Neno nashukuru hutumika katika maamkuzi.
Kwa mfano:
- Ulilalaje? — Nililala vyema, nashukuru.
- Umeamkaje? — Nimeamka vizuri, nashukuru.
Shukrani hizi huwa ni kwa Mwenyezi Mungu.