Chapter 1.1 (Kiswahili 4)

Kusikiliza na Kuzungumza: Matamshi bora

Kipindi cha 1: Silabi na vitanzandimi vyenye sauti p na b

Shughuli ya 1: Kutamka na kutambua silabi za sauti p

  1. Tamka silabi hizi baada ya mwalimu.
    ​pa, pe, pi, po, pu
  2. Tambua silabi za sauti p katika maneno haya.
    1. pasi
    2. pewa
    3. pika
    4. ponda
    5. punda
  3. Tambua silabi za sauti p katika maneno ya sentensi zilizo kwenye ubao.

Shughuli ya 2: Kutamka na kutambua silabi za sauti b

  1. Tamka silabi hizi baada ya mwalimu.
    ​ba, be, bi, bo, bu
  2. Tambua silabi za sauti b katika maneno haya
    1. baba
    2. mkebe
    3. bilauri
    4. boma
    5. sebule
  3. Tambua silabi za sauti b katika maneno ya sentensi zilizo kwenye chati ya mwalimu.

Shughuli ya 3: Kujadili michoro na kusikiliza

  1. Tambueni majina ya michoro hii mkiwa wawiliwawili. Tamkeni majina hayo.
  2. Sikilizeni maneno yenye sauti p na b yaliyorekodiwa kwenye rununu ya mwalimu.
  3. Tamkeni maneno mliyosikiliza.

Je, unajua?

Maneno uliyotambua katika michoro ya shughuli ya 3 yana sauti p na b. Sauti hizi mbili zinakaribiana kimatamshi. Maneno hayo yana maana tofauti. Maneno hayo huitwa vitate.

  1. Tambueni vitate vya sauti p na b katika mraba huu mkiwa katika vikundi kwa kubonyeza sarafu ya kwanza na ya mwisho.
  1. Tumieni vitate mlivyotambua katika mraba kutunga sentensi sahihi.
    Mfano: Mtoto alimpata bata jikoni. 
  2. Sikiliza mwenzako akisoma sentensi mlizotunga. Karirini kwa zamu na kwa haraka sentensi mlizotunga.

Je, unajua?

Sentensi mlizotunga kwa kutumia vitate huitwa vitanzandimi.

Kazi ya ziada

Jadiliana na mlezi au mzazi wako kuhusu umuhimu wa vitanzandimi. Waeleze wanafunzi wenzako darasani mliyojadiliana.

Kipindi cha 2: Silabi na vitanzandimi vyenye sauti t na d

Shughuli ya 1: Kutamka na kutambua silabi za sauti t

  1. Tamka silabi hizi baada ya mwalimu.
    ​ta, te, ti, to, tu
  2. Tambua silabi za sauti t katika maneno haya.
    1. kitanda
    2. uteo
    3. koti
    4. tonge
    5. tunda
  3. Tambua silabi za sauti t katika maneno ya sentensi zilizo kwenye tarakilishi ya mwalimu.

Shughuli ya 2: Kutamka na kutambua silabi za sauti d

  1. Tamka silabi hizi baada ya mwalimu.
    ​da, de, di, do, du
  2. Tambua silabi za sauti d katika maneno haya.
    1. seredani
    2. debe
    3. dirisha
    4. donge
    5. mdudu
  3. Tambua silabi za sauti d katika maneno ya sentensi zilizo kwenye ubao.

Shughuli ya 3: Kusoma vitanzandimi

  1. Someni vitanzandimi hivi kwa usahihi mkiwa katika vikundi.
    1. Tunda kubwa lilidunda chini.
    2. Nilipomtuma Mutuma alikutana na duma njiani.
    3. Toa kitambaa chenye doa mfukoni.
  2. Mwanafunzi mmoja arekodi usomaji wa wenzake kwa kutumia rununu ya mwalimu au tarakilishi.
  3. Sikilizeni na mtamke kwa haraka na kwa usahihi sentensi zilizorekodiwa.
  4. Undeni vitanzandimi sahihi mkitumia maneno yenye sauti t na d.
    ​Vikaririni kwa haraka na sauti.

Kazi ya ziada

Mtajie mlezi au mzazi wako vitanzandimi vitatu vyenye sauti t na d ulivyojifunza. Vikaririni pamoja.

Kipindi cha 3: Silabi na vitanzandimi vyenye sauti k na g

Shughuli ya 1:Kutamka na kutambua silabi za sauti k

  1. Tamka silabi hizi baada ya mwalimu.
    ​ka, ke, ki, ko, ku
  2. Tambua silabi za sauti k katika maneno haya.
    1. kabati
    2. keti
    3. kinu
    4. kochi
    5. kufuli
  3. Tambua silabi za sauti k katika maneno ya sentensi zilizo kwenye ubao.

Shughuli ya 2: Kutamka na kutambua silabi za sauti g

  1. Tamka silabi hizi.
    ​ga, ge, gi, go, gu
  2. Tambua silabi za sauti g katika maneno haya.
    1. gawa
    2. gesi
    3. ufagio
    4. goti
    5. gunia
  3. Tambua silabi za sauti g katika maneno ya sentensi zilizo kwenye chati ya mwalimu.

Shughuli ya 3: Kuunda vitanzandimi

  1. Sikilizeni mwalimu akisoma maneno haya. Tamkeni baada ya mwalimu.

A

B

koti

goti

ukali

ugali

koma

goma

  1. Mwanafunzi mmoja ayarekodi matamshi yenu kwa kutumia tarakilishi, rununu au rekoda.
  2. Mkiwa wawiliwawili, undeni vitanzandimi vyenye sauti k na g kwa kutumia maneno yaliyorekodiwa.
  3. Mwambie mwenzako avisome kwa haraka vitanzandimi mlivyounda.

Kazi ya ziada

  1. Mkaririe mlezi au mzazi wako vitanzandimi vitano ulivyojifunza shuleni.
  2. Mwambie akurekodi kwa kutumia rununu au tarakilishi.

Kipindi cha 4: Silabi na vitanzandimi vyenye sauti ch na j

Shughuli ya 1: Kutamka na kutambua silabi za sauti ch

  1. Tamka silabi hizi.
    ​cha, che, chi, cho, chu
  2. Tambua silabi za sauti ch katika maneno haya.
    1. chakula
    2. cherehani
    3. chiriku
    4. choo
    5. chumba
  3. Tambua silabi za sauti ch katika maneno ya sentensi zilizo kwenye ubao.

Shughuli ya 2: Kutamka na kutambua silabi za sauti j

  1. Tamka silabi hizi.
    ​ja, je, ji, jo, ju
  2. Tambua silabi za sauti j katika maneno haya.
    1. jagi
    2. jembe
    3. jiko
    4. jokofu
    5. jua
  3. Tambua silabi za sauti j katika maneno ya sentensi zilizo kwenye ubao.

Shughuli ya 3: Kuunda vitanzandimi

  1. Soma maneno haya kwa sauti. Wanafunzi wenzako wakusikilize.

A

B

chuma

juma

chana

jana

changa

janga

chumba

jumba

  1. Mmoja wenu darasani ayarekodi matamshi yenu kwa kutumia rununu ya mwalimu.
  2. Mkiwa katika vikundi, undeni vitanzandimi ubaoni mkitumia maneno yaliyorekodiwa.
  3. Someni vitanzandimi mlivyounda kwa sauti na kwa haraka.

Kazi ya ziada

Mtajie mlezi au mzazi wako vitanzandimi viwili vyenye sauti ch na j. Vikaririni pamoja.

Please wait