Mkiwa wawili, tazameni mchoro huu.

Maswali
- Unaona nini katika mchoro huo.
- Watu hufanya nini shuleni?
- Ukienda shuleni utawaona nani?
- Utapata vitu gani shuleni?
- Wewe unasoma katika shule gani?
- Shule yenu ina vifaa gani?
Sauti /g/
Mkiwa wawili, tazameni michoro hii.
Maswali
- Taja majina ya michoro hiyo.
- Tamka herufi ya kwanza ya majina hayo.
- Tamka sauti /g/ baada ya mwalimu.
- Tamkeni sauti /g/ mkiwa wawili.
- Tamka sauti /g/ peke yako.
Zoezi
Mkiwa wawili, jibuni maswali haya.
- Andika herufi g katika daftari lako.
- Andika herufi G katika daftari lako.
- Tamka sauti /g/ kwa usahihi.
Silabi za herufi g
Mkiwa wawili, tamkeni irabu hizi.

Mkiwa wawili, tamkeni silabi hizi zenye sauti /g/.

Tamka silabi hizi na maneno yenye sauti /g/.
Mkiwa watatu, tamkeni maneno haya.
