Matamshi bora – Silabi na vitanzandimi
Sauti: d na nd, ch na sh, j na nj, g na ng
Shughuli 1: Kutambua silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana
- Tazameni picha hizi mkiwa wawiliwawili. Tajeni silabi za maneno ya picha hizi.
- Sikiliza maneno yatakayotamkwa na mwalimu au kifaa cha kidijitali.
- Ni silabi zipi zilizo na sauti zinazokaribiana katika maneno uliyoyasikiliza? Zitaje.
- Ukishirikiana na mwenzako, tajeni silabi zenye sauti zinazokaribiana katika maneno yafuatayo:
d
nd
ch
sh
doa
poda
dada
dau
duarandoa
ponda
danda
ndau
nduarachoka
chati
chombo
chali
pichashoka
shati
shombo
shali
pishaj
nj
g
ng
jaa
kuja
fuja
wajanjaa
kunja
punja
wanjagoma
fuga
soga
gogongoma
funga
songa
gongo- Mwonyeshe mwenzako silabi za sauti d na nd, ch na sh, j na nj, g na ng katika maneno hayo.
Shughuli 2: Kutamka silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana kimatamshi
- Ukiwa na mwenzako, tamkeni silabi zifuatazo kwa zamu:
- Silabi za sauti d na nd
da, de, di, do, du
nda, nde, ndi, ndo, ndu - Silabi za sauti ch na sh
cha, che, chi, cho, chu
sha, she, shi, sho, shu - Silabi za sauti j na nj
ja, je, ji, jo, ju
nja, nje, nji, njo, nju - Silabi za sauti g na ng
ga, ge, gi, go, gu
nga, nge, ngi, ngo, ngu
- Silabi za sauti d na nd
- Jirekodini mkitamka silabi kisha msikilize matamshi yenu.
- Mkielekezwa na mwalimu, rekebisheni matamshi yenu pale panapostahili.
Shughuli 3: Kutamka vitanzandimi
- Sikilizeni vitanzandimi vilivyorekodiwa katika chombo cha kidijitali.
- Ukiwa na mwenzako, tamkeni vitanzandimi vifuatavyo kwa zamu:
- Ndoa isiyokuwa na doa hudumu.
- Mjomba alikunja mkunjo mwingine jana.
- Chombo kilichotumiwa kupikia samaki kinanuka shombo.
- Mtema kuni alichoka baada ya kuchanja kuni kwa shoka.
- Shehe aliyevalia shali amelala chali.
- Ngoma iliyotumiwa na wagomaji ilipatikana baada ya mgomo kusitishwa.
- Vipodozi vya poda vilipondwapondwa na punda.
- Udongo wa Odongo umeingiwa na mdudu mdogo.
- Mja aliyekuja kwetu alikunjua nguo zilizokunjika.
- Msichana alitishwa na picha ya chatu kwenye shati.
- Mkiwa katika vikundi, tambueni sauti zinazokaribiana katika kila kitanzandimi.
Shughuli 4: Kuunda vitanzandimi
- Shirikiana na mwenzako kuunda vitanzandimi ukitumia maneno haya:
- goma/ngoma
- chati/shati
- doa/ndoa
- poda/ponda
- choka/shoka
- kuja/kunja
- jaa/njaa
- gogo/gongo
- Shirikiana na mwenzako kuvikariri darasani vitanzandimi mlivyounda ili wenzenu wavisikilize na kutoa maoni.
Changamka
Tumia kifaa cha kidijitali kujirekodi ukitamka vitanzandimi ulivyounda kisha mwalimu atathmini matamshi yako.