Kusikiliza na kujibu – Mjadala
Durusu chapuchapu
Ulijifunza kuhusu kusikiliza na kujibu mazungumzo na mahojiano katika gredi za awali.
Jibu maswali haya ili kudurusu uliyojifunza.
- Ni nini tofauti kati ya mahojiano na mazungumzo ya kawaida?
- Mweleze mwenzako mambo matatu muhimu ya kuzingatia unaposhiriki:
- mazungumzo
- mahojiano.
Katika sehemu hii, utajifunza kuhusu kusikiliza na kujibu mjadala.
Kichocheo
- Je, wanafunzi wanajadiliana kuhusu nini?
- Je, unafikiri wanafunzi waliosimama wanafanya nini? Toa sababu ya maoni yako.
Shughuli ya 1
Ukishirikiana na mwenzako:
- Sikilizeni au mtazame mjadala kati ya mwalimu na wanafunzi darasani mkielekezwa na mwalimu.
- Tambueni vipengele vinavyoonyesha kuwa Mwanafunzi II alisikiliza mjadala na mvieleze. Zingatieni mambo yafuatayo:
- kumtazama mzungumzaji,
- kutambua hoja ya kujibu mjadala,
- kuchagua msimamo utakaotetea.
- Elezeni msimamo wa washiriki wafuatao katika mjadala mliosikiliza au mliotazama.
- Mwanafunzi I
- Mwanafunzi II
- Mwalimu
- Toeni sababu ya maelezo yenu ya swali la 3 (a) – (c).
Shughuli ya 2
Ukiwa na mwenzako:
- Sikilizeni au mtazame tena mjadala kati ya mwalimu na wanafunzi.
- Tambueni vipengele ambavyo wanafunzi walizingatia katika kuchangia mjadala na mvieleze. Rejeleeni mambo yafuatayo:
- kujibu wakati ufaao,
- kutetea msimamo,
- kujikita katika kiini cha mazungumzo,
- kutumia lugha ya adabu na shawishi,
- kuzungumza kwa ukakamavu.
Shughuli ya 3
Ukiwa na wenzako:
- Shirikini mjadala: Usafi wa mazingira ndio unaozuia kuenea kwa maradhi. Zingatieni hatua zifuatazo:
- Jigaweni katika vikundi viwili darasani; kimoja cha kuunga mkono mjadala na kingine cha kupinga.
- Tayarisheni hoja za kuunga mkono au kupinga mjadala.
- Chagueni viongozi wa kuwaelekeza. Viongozi hao ni mwenyekiti, makatibu, mlinda nidhamu na mtunza wakati.
- Fanyeni mjadala darasani kuhusu mada mliyopewa.
- Waombeni makatibu kusoma muhtasari wa hoja.
- Mpeni mwamuzi nafasi ya kutangaza matokeo.
- Nakilini daftarini jedwali lililo katika ukurasa wa 3. Mwombe mwenzako alikamilishe kuonyesha ni kwa kiasi gani ulizingatia vipengele vya mjadala.
Tathmini
Weka alama inapofaa ili kutathmini uwezo wa mwenzako wa kuzingatiavipengele vifaavyo katika kusikiliza na kuchangia mjadala.
Umilisi unaotathminiwa | Kila wakati | Wakati mwingi | Wakati mwingine | Nadra |
Alijikita katika kiini cha mjadala. | ||||
Alitetea msimamo wake. | ||||
Alitumia lugha ya adabu na shawishi. | ||||
Alizungumza kwa ukakamavu. | ||||
Alijibu wakati ufaao. | ||||
Jina la mwanafunzi: | Tarehe: | |||
Maoni ya mwalimu: | Sahihi: | Tarehe: |
- Wasilisha jedwali kamili kwa mwalimu akupe maoni yake.
Wazo bainifu
- Nimegundua kuwa ili kusikiliza na kujibu mjadala, washiriki huzingatia vipengele vifuatavyo:
- kusikiliza kwa makini,
- kumtazama mzungumzaji,
- kutambua hoja ya mjadala,
- kutambua msimamo utakaoutetea,
- kutetea msimamo wako,
- kujibu wakati ufaao,
- kujikita katika kiini cha mazungumzo,
- kutumia lugha ya adabu na shawishi,
- kuzungumza kwa ukakamavu.
- Hatua zinazofuata huzingatiwa katika mjadala:
- kuteua mada ya mjadala,
- kujigawa katika vikundi viwili; kimoja cha kuunga mkono na kingine cha kupinga mjadala,
- kutayarisha hoja za kuunga mkono au kupinga mjadala,
- kuchagua viongozi wa kuelekeza mjadala. Viongozi hao ni:
- Mwenyekiti – huongoza mjadala.
– hutangaza matokeo. - Makatibu – kila upande huwa na katibu wake ambaye hunakili hoja zinazotolewa.
- Mlinda nidhamu – huhakikisha nidhamu inadumishwa katika mjadala.
- Mtunza wakati – huhakikisha watu wanazingatia muda uliowekwa kwa mjadala.
- Mwenyekiti – huongoza mjadala.
Kazi mradi
Mkielekezwa na mwalimu, fanyeni kazi mradi ifuatayo:
- Undeni chama cha mjadala darasani.
- Chagueni viongozi watakaowaelekeza.
- Pangeni ratiba ya mijadala:
- Baina yenu darasani,
- Kati ya gredi yenu na gredi zingine.
- Pendekezeni mada ambazo mtazijadili.
- Fanyeni utafiti kuhusu mada hizo.
- Wasilisheni hoja zenu wakati wa mijadala.
Tembea na majira
- Sakura mtandaoni video kuhusu mjadala wa wanafunzi.
- Itazame na uisikilize video hiyo.
- Waeleze wenzako darasani mjadala ulihusu nini.
- Jadili na wenzako mambo yaliyokuvutia katika mjadala uliotazama.