Chapter 1.1 (Kiswahili 3)

Shambani

Mkiwa wawili, tazameni michoro hii.

a
b
ch
d
  1. Unaona nini kwenye michoro hii?
  2. Watu hawa wako wapi?
  3. Watu hawa wanafanya nini?
  4. Watu hawa wanatumia vifaa gani?
  5. Wewe hufanya kazi gani shambani?

Sauti mbili tofauti zinazotamkwa pamoja /bw/

Sauti /bw/

Mkiwa wawili, tazameni michoro hii.

a
b
ch
d

Maswali ya makundi

  1. Taja majina ya michoro hii.
  2. Tamka herufi ya kwanza pekee ya majina hayo.
  3. Tamka sauti /bw/ baada ya mwalimu.
  4. Tamkeni sauti /bw/ mkiwa wawili.
  5. Tamka sauti /bw/ peke yako.

Zoezi

Mkiwa wawili, jibuni maswali haya.

  1. Andika herufi bw katika daftari lako.
  2. Andika herufi BW katika daftari lako.
  3. Tamka sauti /bw/ kwa usahihi.

Silabi za herufi bw

Mkiwa wawili, tamkeni irabu hizi.

Mkiwa wawili, tamkeni silabi hizi zenye sauti /bw/.

Tamka maneno haya yenye sauti /bw/.

  1. Jiwe ku.
  2. Mbwa anaka.
  3. Hili niwa la maji.
Please wait